Harusi ya mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi sasa ni uhakika itakuwa Juni 30 na itafanyika kwao Rosario, Argentina yeye akifunga ndoa na mzazi mwenzake na mpenzi wake tokea wakiwa shule, Antonella Roccuzzo.
Awali ilielezwa, beki Gerard Pique rafiki wa Messi hakualikwa kwa kuwa mkewe Shakila haelewani na bibi harusi mtarajiwa.
Lakini kinachoonyesha kuwashangaza wengi ni kutoalikwa hata kwa Kocha Luis Enrique ambaye ameamua kuondoka Barcelona lakini madaktari wa Barcelona na kocha mpya, Joaquin Valdes ni kati ya waalikwa.
Sherehe za harusi hiyizo zitafanyika katika hoteli ya Pullman ambayo tayari vyumba 250 vimelipiwa na baadhi ya wageni wamekuwa ni siri.
Pia imeelezwa viongozi wengi wa klabu ya Barcelona hawajaalikwa na Sergio Aguero ni kati ya walioalikwa.
Taarifa nyingine zimeeleza jumla ya watu 21 kutoka katika kikosi cha Barcelona wamelikwa na tayari maandalizi ya “kufa mtu” yameishaanza.
Un buteur prolifique, Messi est connu pour sa finition, son positionnement, ses réactions rapides et sa capacité à effectuer des courses offensives pour battre la ligne défensive.
ReplyDelete