June 21, 2017



Everton inakuwa ni klabu ya kwanza kutoka nchini England katika kipindi cha hivi karibuni kutembelea ukanda huu wa Afrika Mashariki kwa ziara ya kimichezo.

Ni mara chache kusikia vilabu ya EPL vikija Afrika kwa ajili ya mechi za maandalizi ya msimu mpya dhidi ya timu wenyeji ambapo mara nyingi nchi za China, Japan na Marekani ndizo zimekuwa zikitembelewa zaidi.
Mwaka 2011 klabu ya Tottenham ilienda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya ambapo ilicheza dhidi ya magwiji wa nchi hiyo, Orland Pirates na Kaiser Chiefs. 

Mwaka uliofuata, Manchester United nao walitembelea nchini humo ambapo walicheza dhidi ya vilabu vya Amazulu na Ajax Cape Town huku bila kusahau ziara ya hivi karibuni ya Crystal Palace ya mwaka 2015 nchini humo ambapo pia walicheza na vilabu wenyeji vya Super Sport United na Ajax Cape Town.
Sio jambo la kushangaza kuona vilabu vya EPL vikimiminika nchini Afrika Kusini mwaka hadi mwaka kutokana na nchi hiyo yenye maendeleo makubwa ya kiuchumi kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuandaa fainali za michuano ya Kombe la dunia ya mwaka 2010 kwa mafanikio makubwa tofauti na matarajio ya wengi.

Kombe la dunia liliifungulia Afrika Kusini milango kwa vilabu vingi kutoka barani Ulaya kwenda kutembelea nchini humo kitu ambacho pia kitatokea Tanzania kwani ujio wa Everton utatoa fursa ya kipekee kwa Tanzania kujitangaza kimataifa katika soka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic