June 19, 2017


Hatimaye Mtemi Ramadhani amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Mtemi amechukua fomu hiyo leo akisindikizwa katika ofisi za TFF Karume jijini Dar es Salaam na baadhi ya wachezaji wa zamani.

Atakaochuana nao Mtemi ni Geofrey Nyange 'Kaburu', Michael Wambura na Mulamu Ng'ambi.
Mmoja wa wanaowania nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF.


Mtemi alikuwa mshambuliaji hatari wa Simba pia Taifa Stars wakati huo akikipiga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV