June 19, 2017Beki mgumu wa Yanga, Vincent Bossou, raia wa Togo, ameweka wazi kuwa, atajua hatma ya maisha yake ndani ya kikosi hicho kama atakuwepo kwa msimu ujao au la baada ya kurejea nchini akitokea kwao alipokwenda kwa ajili ya mapumziko baada ya kumalizika kwa ligi.

Bossou ni miongoni mwa wachezaji wa kimataifa wa Yanga ambao wamemaliza muda wao wa kuitumikia klabu hiyo baada ya mkataba wake wa miaka miwili kumalizika.

Bossou amesema kuwa mpaka sasa hajatambua lolote kuhusu yeye kurejea ndani ya kikosi hicho kutokana na kutozungumza na viongozi wa timu hiyo tangu mkataba wake ulipomalizika.

“Sifahamu lolote kuhusu kurejea ndani ya Yanga kwa sababu sijaongea na viongozi tangu mkataba wangu ulipofika ukingoni, kwa sasa nawasubiri wao waniite ili tuanze kujadili juu ya mkataba mpya.

“Muda huu nipo mapumzikoni nyumbani, najipa muda zaidi wa kukaa na familia sambamba na kufanya mazoezi ili msimu ujao niwe na kiwango kikubwa zaidi ya kile ambacho nilikionyesha msimu uliopita wa ligi,” alisema Bossou.


SOURCE: CHAMPION

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV