June 21, 2017Beki wa kushoto wa Simba, Mohammed Zimbwe amefunguka kuwa kamwe hatokubali kuona anapokonywa nafasi  yake kirahisi na mchezaji yoyote wa timu hiyo.

Tshabalala ameyasema hayo kufuatia Simba kumsajili aliyekuwa beki wa Mbao FC ya Mwanza atakayeshindana naye, Jamal Mwambeleko, kwa mkataba wa miaka miwili.

Zimbwe maarufu kama Tshabalala ambaye ametajwa kama mchezaji bora wa Simba msimu huu, alisema kuwa siku zote amekuwa akifuata utaratibu alijiwekea katika mchezo wa mpira kwa kuwa amekuwa hapendi kuona akirudishwa nyuma na mtu atakayekuwa anataka kuchukua nafasi yake.

“Hii yote imetokana na suala zima la nidhamu na kujituma kwa sababu siku zote nimekuwa sipendi kuona nikivunja miiko yangu  katika mchezo wa soka ambayo nimejiwekea, kwa sasa natakiwa niendelee kufanya zaidi ya nilipofikia ili nizidi kuwa bora.

“Unajua mimi ni mchezaji na sitakiwi kuhofia mchezaji yoyote ambaye anakuja katika timu yetu, najua kuwa hivi sasa timu inafanya usajili kwa ajili ya msimu ujao, naamini ushindani wa namba utakuwa mkubwa ila niseme tu kwa upande wangu kama nitaendelea kuwa mzima basi sitokubali kupokonywa namba yangu,” alisema Tshabalala ambaye pia ni mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV