June 26, 2017Klabu ya Kagera Sugar ya Kagera, imeonyesha kudhamiria kuimarisha kikosi chake msimu ujao wa ligi kufuatia kumuwinda mshambuliaji wa Mwadui FC, Joseph Kimwaga.

Kagera Sugar inataka kumsajili Kimwaga ambaye aliwahi kuzichezea klabu za Azam FC na Simba ili kuongeza nguvu katika kikosi hicho huku ikiwa tayari imeshasajili wachezaji kadhaa akiwemo beki Juma Nyosso na kiungo Peter Mwalianzi wa African Lyon.

Katibu wa Kagera Sugar, Mohamed Hussein amesema, kwa sasa wapo katika mazungumzo ya kuingia mkataba na mshambuliaji huyo kwa lengo la kuimarisha kikosi chao.


“Tupo katika mazungumzo mazuri na Kimwaga kwa ajili ya kumsajili katika msimu ujao wa ligi kuu ambapo kwa sasa yupo hapa Kagera kwa ajili ya mazungumzo na tukishakubaliana, basi atasaini,” alisema Hussein.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV