June 20, 2017Kiungo nyota wa Everton, Morgan Schneiderlin ameamua kutangulia nchini.

Schneiderlin yuko nchini kwa ajili ya honeymoon baada ya siku chache kufunga ndoa.Sasa ametua nchini kula raha na mpenzi wake na ametupia picha mtandaoni akiwa mbugani.

Watanzania watapata bahati ya kumshuhudia Schneiderlin akiichezea Everton katika mechi yake ya kwanza barani Afrika ambayo itapigwa Julai 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Everton itakuja nchini kucheza na Gor Mahia katika mechi ya kirafiki ya kimataifa.


Gor Mahia ndiyo mabingwa wa SportPesa Super Cup.


1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV