June 28, 2017



Kocha mpya wa Lipuli FC ya mkoani Iringa, Selemani Matola, ameeleza kuwa, tayari ameshaanguka wino wa kuitumikia Lipuli kwa mkataba wa mwaka mmoja na kudai kuwa, anahitaji kukifanyia mabadiliko kikosi hicho kwa kuhakikisha anasajili wachezaji vijana.

Lipuli ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda daraja msimu uliopita, ikiwa ni pamoja na Njombe Mji ya Iringa na Singida United baada ya kufanya vyema Ligi Daraja la Kwanza.

 Matola amesema kuwa, baada ya kufanikiwa kusaini mkataba katika klabu hiyo, moja ya kazi atakazoanza nazo ni kuhakikisha anakifanyia uboreshaji kikosi hicho kwa kusajili wachezaji vijana huku akibakiza wachache walioipandisha timu daraja.

“Natarajia kwenda Iringa wakati wowote, kwa sasa kuna programu ambayo nahitaji kuifanya kwa ajili ya suala zima la usajili, ya kwanza nitaanza nayo hapa na nyingine nitaenda kuifanyia Iringa lakini nitaangalia ndani ya siku mbili hizi ndiyo nitaweza kutoa majibu rasmi.

“Leo natarajia kukutana na uongozi wangu kwa ajili ya kupanga mikakati zaidi kwa ajili ya usajili wa timu kwani nahitaji kukifanyia uboreshaji kikosi kwa kusajili wachezaji wenye uwezo watakaoisaidia timu hapo baadaye.

“Nitaangalia wachezaji waliopandisha timu kwa kuanza na wale 15 aliowapendekeza mwalimu aliyepita wabaki nitawachuja na kuona kama wananifaa ama la,” alisema Matola.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic