June 28, 2017Beki mpya wa Simba, Shomari Kapombe amesema kurejea kwao akiwemo Emmanuel Okwi ni sawa na kuirejesha Simba ya enzi za Patrick Mafisango.
Kapombe ambaye amerejea Simba akitokea Azam FC, amesema amefurahi kwa kuwa anaamini kikosi chao kitakuwa imara na kinachotakiwa ni ushirikiano tu.
Mafisango alikuwa kiungo wa Simba raia wa DR Congo na alifariki kwa ajali ya gari mwaka 2012.
“Itakuwa ni sawa na Simba ya kipindi cha kina Mafisango, wanaweza kuongeza nguvu tu katika ulinzi zaidi.
“Lakini hii itakuwa ni Simba yenye ushindani mkubwa na kama tutashirikiana na kujituma, ninaamini tutafanya vizuri,” alisema.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV