June 23, 2017





Na Saleh Ally
KAWAIDA mashabiki ni watu wenye upendo na vitu na si utu. Hii imekuwa ikijengeka katika klabu nyingi hasa za dunia ya tatu, yaani katika nchi nyingi za Afrika, Asia na Amerika Kusini.

Hata Ulaya, kuna baadhi hili linatokea la mashabiki kuonyesha wanavutiwa na klabu yao tu na si kujali utu wa wachezaji husika ambao walikuwa au wapo katika klabu au timu zao.

Haruna Hakizimana Niyonzima ni Mnyarwanda ambaye alikuja nchini kutafuta maisha baada ya kucheza kwao Rwanda kwa mafanikio makubwa akiitumikia APR baada ya kuchipukia Magharibi mwa nchi ya Rwanda akiwa na Entecell.

Wakati anajiunga Yanga misimu sita iliyopita, APR moja ya klabu tajiri kwa Afrika Mashariki ilitaka kumzuia kwa kuwa inajua umuhimu wake. Yeye alisisitiza angependa kwenda Yanga ili kupata changamoto mpya kwa kuwa Rwanda ameshinda kila kinachotakiwa kushinda kwa ngazi ya taifa.

Alitua Yanga na akawathibitishia Wanayanga na Watanzania wapenda soka kuwa yeye ni mchezaji bora na mwenye mchango mkubwa kwa kuwa ndani ya kipindi cha miaka sita, ameipa Yanga ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara nne, Kombe la Kagame mara moja, ubingwa wa Kombe la Shirikisho na kufika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Niyonzima ameondoka Yanga, taarifa zinaeleza anakwenda kujiunga na Simba. Hili ni jambo baya kabisa kwa baadhi ya mashabiki wasio na hisia sahihi za ushabiki uliochanganyika na ubinadamu.


Hawa ni mashabiki ambao zaidi wanalenga furaha yao, hawaamini mchezaji naye ni mwanadamu. Ana mipango au ndoto zake, anataka kufikia au kupiga hatua na kulipata jambo fulani.

Uhalisia uko hivi; Niyonzima amemaliza mkataba na Yanga. Baada ya hapo mazungumzo ya mkataba mpya yakaanza, yeye akaweka dau mezani. Yanga wakaomba kupunguziwa, akafanya hivyo lakini mwisho inaonekana hata hapo hawawezi kufikia.

Mwisho Yanga wamekubali Niyonzima aende na uongozi umetangaza huku ukimtakia kila la kheri. Kwangu naona ni jambo zuri kuachana vizuri na mtu aliyefanya kazi na wewe kwa ushirikiano wa juu.

Mmoja wa mashabiki wa Yanga, yeye ameamua kumaliza hasira zake kwa kuchoma jezi ya Niyonzima na wako wachache wenye ushabiki ninaoufananisha na ule msemo wa “mashabiki mandazi”, wamekuwa wakimuunga mkono.

Wako wanaotoa hoja dhaifu kama ile, shabiki huyo amechoma jezi aliyonunua yeye. Jambo ambalo linaonyesha matofali ya hoja zao ni dhaifu hivyo haziwezi kujengwa sahihi.

Leo mtu akinunua jezi ya timu, akaichoma hata yake, haliwezi kuwa jambo la kawaida. Linaonyesha dharau ya wazi na maumivu ya moyo. Unaweza kununua bendera ukaichoma kwa madai umetoa fedha yako kuinunua? Jaribu uone!
Wale wanaomuunga mkono yule shabiki maandazi, wanapaswa kujitambua safari ya Yanga ni ile ambayo mimi, wewe na yule shabiki mandazi tuliikuta. Nina hakika tutaiacha inaendelea baada ya mwisho ya siku zetu.

Ili safari iendelee, lazima watu wapite kama ambavyo Niyonzima anapita. Hiyo ndiyo maana ya klabu, wanaingia na wanatoka halafu wanaingia wengine na msimu ujao, utaona kutakuwa na kiungo mwingine staa Yanga kwa kuwa Niyonzima atakuwa ameacha nafasi.

Anayeshangazwa na Niyonzima kuhama leo, ni mgeni wa mpira. Vipi APR hawakuchoma jezi zake, maana yake ina mashabiki wanaojitambua zaidi kuliko Yanga?

Mashabiki hao hawataki kuelezwa, eti kila anayesema anaonekana ni msaliti na wanajenga hisia za kuogopwa, upuuzi mtupu!

Yanga ni klabu inayoheshima, ina mashabiki wengi wanaojitambua, hivyo si vema kuwaadhibu kupitia mashabiki mandazi wachache kama huyo aliyechoma jezi pamoja na wenzake wachache wasiojitambua.

Anayemuita Niyonzima mzee kwa miaka 29 aliyonayo au hata kama ana 33, bado atakuwa anajidanganya kwa kuwa wenye umri huo kama Thabani Kamusoko, Kelvin Yondani, Nadir Ally Haroub ni kati ya wachezaji wanaofanya vizuri kabisa Yanga.

Lazima mjue Niyonzima ni mwanadamu, ana familia yake, ana mipango yake na angehitaji maslahi bora kokote aendako.
Kutoka Yanga kwenda Simba au Simba kwenda Yanga wala si jambo geni, halijaanza leo na ndiyo maana taarifa za Ajibu kwenda Simba zimeenea na hakuna aliyechoma jezi yake.

Edibily Lunyamila, Hamisi Gaga, Mohammed Hussein, Said Mwamba ‘Kizota’, Athumani China, Akida Makunda ni kati ya wachezaji bora waliotoka upande mmoja kwenda mwingine na maisha yaliendelea.
Mpeni Niyonzima heshima yake, acheni ulimbukeni wa kutaka kuonekana au kujionyesha kwa kufanya upuuzi mkitumia kivuli cha ushabiki wa klabu ya Yanga, huo ni ushabiki mandazi.


5 COMMENTS:

  1. Hiyo jezi ni ya njano tu na sio jezi ya Yanga, hata wewe umeingia mkenge? Siamini ktk watu ninao amini wapo makini wewe nilikuwa naamini upo makini sana na ndio maana nafuatilia blog yako lkn sasa wanitia shaka. Ila kila mtu ana maoni na mawazo yake usiwahukumu bila kujua chanzo yawezekana wameumia na wanashindwa kuiona hiyo jezi kwake maana itamuumiza ameamini bora aichome sasa kosa liko wapi? Si kila jambo ni habari kubwa kaka. Naamini kalamu yako bado muhimu sana ktk fani yako na kwa Taifa kila lakheri na pole kama nitakuwa nimekukwaza

    ReplyDelete
  2. helewa ki2 kimoja kaka mashabiki awachani jez kwavle nyionzima kaondoka yanga wamekasiriki kisa timu anayotakakwendando tatzo kubwa kwa mashabiki iyo imewai kutokea ata kwamashabiki wa Barcelona FIGO alipoenda madrid kwaiyo ilo alinishangaz sana ata mashabik wa Liverpool kunakipind walichoma jez za Gerald alivotaka kwenda Chelsea

    ReplyDelete
  3. Huo ni ushabiki maandazi tuu..mbona jezi ya ajib haijachomwa..inamaana mashabiki wa simba hawajaumia!! Mtu anataka hela..mpeni hajakataa kuchezea timu yenu..au mlifikiri Mlifunga nae ndoa kwamba ameshakuwa mali ya Yanga.. Hizo ni fikra za kizamani sana.. mnaamini kwamba hamtapata mwingine..kutafuta wachezaji ni shida mkimpata basi hatoki mpaka wazeekee humo.. Hilo jambo la kuchoma jezi limenikera sana na linaonyesha jinsi gani ana mawazo mgando..kwamba hakitaweza kupatikana kama hiki..basi wapeni hela sio mnachoma jezi tuu..

    ReplyDelete
  4. KATIKA WAANDISHI MAKANJANJA BASI WEWE KILAZA SALEH ALLY NI WA KWANZA.mWANDISHI GANI HATUMII AKILI KUANDIKA KISA ETI NI MWANACHAMA WA SIMBA!kUMBUKA WEWE ULIKUWA UNAPAMBANA NA MALINZI MUDA WOTE KWA VILE AMETOKA YANGA NAWE ULITAKA MIJUSI WENZAKO NDIO IKAE TFF,SASA UNARUKIA JAMBO USILOLIFAHAMU KWANI JEZI HIYO IMECHUKULIWA KWA NIYONZIMA AU KUNA MTU KANUNUA KWA KUTUMIA PESA YAKE NA KUICHOMA?
    TUMIA AKILI JAPO NAJUA WEWE NI KILAZA TOKA UKIWA SHULENI,NILISOMA NAWE NAKUJUA FIKA KWANI HATA YULE MWALIMU WETU MLEMAVU ALIKUWA ANAKUCHAPA KILA SIKU KWA KUSHINDWA KUTAMKA NENO KASRI.PUMBA SANA MWENZANGU.

    ReplyDelete
  5. Ufaulu wa darasani haimaanishi wewe ndio kichwa.. WaPo wengi tuu wanapigwa gap na watu ambao darasani hawakuwa wazuri ila wana vipaji vyao.. kama unataka kuthibitisha hilo fuatilia kama Mo au Bakhressa au Aliko Dangote wana PhD za business..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic