Ujio wa klabu kongwe nchini England ya Everton, maandalizi yote yamekamilika.
Julai 13, Everton itashuka kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuwavaa Gor Mahia.
Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba amesema kila kitu kinachohusiana na maandalizi ya ujuo huo, kimekamilika.
“Kila kitu kimekamilika, limebaki ni suala la safari na tunausubiri ujio huo kwa hamu kubwa sana,” alisema Tarimba.
Gor Mahia ilipata nafasi hiyo baada ya kubeba ubingwa wa SportPesa Super Cup kwa kuwafunga AFC Leopards kwa mabao 3-0 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment