June 24, 2017


Uliwahi kusikia kwamba kiungo Ramadhani Singano amegoma kusaini mkataba Azam FC? unaijua sababu?

Wengine wakasema, Singano ameiomba msamaha Simba anataka kurudi, kumbe hawakujua ishu inavyoendelea.

Ishu iko hivi, Singano maarufu kama Messi ataondoka nchini wakati wowote kwenda nchini Morocco kumalizia mipango ya kujiunga na Klabu ya Difaa El Jajida na atapewa mshahara wa dola 2,000 (zaidi ya Sh milioni 4.4), kwa mwezi.

Hivi karibuni, Singano alikataa kuongeza mkataba na Azam FC ambayo sasa imepanga wachezaji kutokuwa na mshahara mkubwa zaidi ya Sh milioni 2.

 Kupitia wakala wale, Singano amekubaliana na kujiunga na El Jajida ambayo imemaliza katika nafasi ya pili kwenye ligi ya Morocco, na taarifa zinaeleza mkataba wake utaisha Julai 8, mwaka huu.

Mohamed El Hamsi ambaye ni mmoja wa wanaoshughulikia safari ya Singano kwenda nchini humo, amesema kila kitu kimekamilika.

 “Kila kitu kimekamilika na Difaa El Jadida imeridhika, sasa tunamsubiri aje kutoka huko Tanzania. Alisema atakula sikukuu, baada ya hapo ataungana nasi huku,” alisema El Hamsi kutoka Morocco.

 “Tunachosubiri ni kwamba amalize mkataba wake Julai 8, baada ya hapo litafuatia suala la mkataba.”

 Singano alijiunga na Azam FC akitokea Simba lakini bado mambo yake hayajawa mazuri sana ndani ya klabu hiyo.

 Hivi karibuni, Azam FC ilibadili utaratibu wake wa uendeshaji na kusababisha wachezaji wake wengi kuondoka akiwemo nahodha John Bocco.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic