June 27, 2017


Mshambuliaji Donald Ngoma ametua jijini Dar es Salaam usiku huu na kupokelewa na mashabiki wa Yanga.


Ngoma amepokelewa na mashabiki hao wa Yanga na kupelekwa mafichoni.

Baadhi ya wanachama wa Yanga waliofika kumpokea walionekana wako makini na kulikuwa na taarifa kwamba Simba nao walitaka kufika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kumchukua.

Lakini taarifa zilieleza kwamba Simba hawakuwa na mpango huo lakini ni kweli wamefanya mazungumzo na Ngoma.

Leo mchana kuna magazeti yalieleza kwamba Ngoma tayari alikuwa jijini Dar es Salaam akiwa amefichwa na Yanga.

Lakini SALEHJEMBE ikagundua Ngoma hakuwa ameingia nchini kama ambavyo ilielezwa..

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV