HAFIDHI |
Bosi wa benchi la ufundi la Simba, Mcameroon, Joseph Omog amevutiwa na kiwango cha mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Hafidhi Musa ambaye amejiunga nayo hivi karibuni akitokea Motema Pembe ya DR Congo.
Musa alionyesha kiwango cha juu katika mchezo alioitumikia Simba dhidi ya Nakuru All Stars ya Kenya jambo ambalo lilimfurahisha Omog na kujikuta akisema kuwa Hafidhi anajua.
OMOG |
Omog alisema amevutiwa na uwezo wa mchezaji huyo na ametoa maagizo ya kufanywa na uongozi juu ya mchezaji huyo.
“Tayari harakati za usajili zimeshaanza na hivi karibuni katika michuano ya SportPesa nimefanikiwa kuona baadhi ya wachezaji ambao nilivutiwa na uwezo wao, lakini aliyenivutia zaidi ni Hafidhi Musa yule mchezaji wetu aliyekuwa amevaa jezi namba 20.
“Ni mchezaji mzuri na ana vitu tofauti ukilinganisha na baadhi ya wachezaji wengine waliocheza mechi hiyo, kwa hiyo kuna maagizo nimeyatoa kwa uongozi dhidi yake, lakini pia nitahitaji kumuona zaidi pindi tutakapoanza mazoezi ya kujiandaa na ligi kuu msimu ujao,” alisema Omog.
Baada ya hivi karibuni kikosi hicho cha Simba kutupwa nje ya michuano ya SportPesa Super Cup wachezaji wa timu hiyo wamepewa mapumziko ya wiki tatu kabla ya kuanza tena maandalizi ya kujiandaa na michuano ya ligi kuu msimu ujao.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment