Mshambulizi nyota, Mbaraka Yusuf sasa ni mali ya Azam FC baada ya kusaini mkataba rasmi wa kuichezea klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.
Awali, Yanga walikuwa na nafasi ya kumsajili wakiweka mezani dau la Sh milioni 50, lakini Azam FC imemnasa kwa Sh milioni 20 kila mwaka, maana yake imetoa Sh milioni 40 kukamilisha usajili wake.
Mbaraka amejiunga na klabu hiyo baada ya kusaini mkataba leo mbele ya Meneja Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohammed.
Kutua kwa Mbaraka maana yake anarithi mikoba ya nahodha wa Azam FC, John Bocco ambaye ameamua kuondoka baada ya kutoridhishwa na majadiliano ya mwisho ya kuongeza mkataba.
Bocco anakwenda Simba na hii itakuwa nafasi nzuri kwa Mbaraka kuonyesha uwezo wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment