Kipa wa zamani wa Barcelona, Victor Valdes amefunga ndoa na mpenzi wake wa sikh nyingi Yolanda Cardona.
Harusi imefanyika katika Kanisa la Santuario de Santa Maria de Montserrat de Pedralbes jijini Barcelona, Hispania na kuhudhuriwa na na nyota wengi wa zamani wa Barcelona ambao walicheza naye pamoja katika kikosi hicho.
Kati ya waliohudhuria ni pamoja na Samuel Eto’o na Seydou Keita pia nahodha wa zamani, Carles Puyol.
Wengine ni pamoja na Eric Abidal na Xavi ambaye alikuwa nahodha wake msaidizi.
0 COMMENTS:
Post a Comment