June 9, 2017




Washindi wa nusu fainali za SportPesa Super Cup zilizofanyika Juni 08, 2017 Jijini Dar es Salaam, wanatarajiwa kukutana uso kwa uso kwenye mechi ya fainali ya kuwania kombe la michuano ya SportPesa Super Cup siku ya Jumapili ya tarehe 11, Juni 2017 itakayochezwa kwenye dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika mechi za nusu fainali, AFC Leopards walipambana na mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara, Klabu ya Yanga na kuwang’oa kwa mikwaju ya penati 4-2 huku Gor Mahia kwa upande wao wakiifungasha virago timu ya Nakuru All Stars FC kufuatia ushindi wa magoli 2-0 ambayo yalitiwa kimiani na mshambuliaji Medie Kagere na George Odhiambo.  

Timu za Yanga na Nakuru All Stars FC ambazo ziling’olewa kwenye hatua ya nusu fainali, zilikabidhiwa medali za shaba na kiasi cha dola za kimarekani 5000 wakati wenzao (Gor Mahia na AFC Leopards) ambao wamefuzu kucheza fainali wakiwania kiasi cha dola za kimarekani 30,000.

Ambapo mshindi kati yao atapata nafasi ya kucheza na timu ya Everton inayoshiriki ligi kuu ya uingereza mnamo Julai 13,2017 uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia mshindano ya SportPesa Super Cup kwa ujumla, Mkurungezi wa Utawala na Utekelezaji SportPesa Tanzania Ndugu Abbas Tarimba alisema; “Michuano ilikuwa migumu ingawa timu zetu za Tanzania zimeaga katika hatua za awali lakini ni nafasi nzuri kwetu kama Tanzania kujipanga vizuri zaidi ili kuboresha sekta ya michezo na kufanya timu zetu kushika nafasi za juu maana kwa sasa tumeweza kutambua changamoto mbalimbali na jinsi ya kuzikabili. 

Pia hii ni nafasi nzuri kwa nchi yetu kuzidi kujitanganza kimataifa, tukiwa na lengo kuu la kuendeleza sekta ya michezo na utalii”. 

“Tutatumia vizuri ujio wa timu ya Everton kuinua soka la Tanzania na kutangaza sekta muhimu ili kuweza kuongeza kipato cha nchi” alisema Ndugu Abbas.

SportPesa ni kampuni nguli ya michezo ya kubashiri inayojulikana kimataifa yenye makao yake makuu nchini Kenya ambayo imeanza rasmi shughuli zake nchini Tanzania Mei 9 mwaka huu na mpaka sasa imeshaingia makubaliano rasmi ya udhamini na vilabu vya Simba, Yanga na Singida United ikiwa imejidhatiti katika kuinua ba kuendeleza sekta ya michezo nchini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic