Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania, (Takukuru) imethibitisha kumshikiria Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na katibu wake, Mwesigwa Silentine kwa
mahojiano ambayo hakuyaweka wazi.
Ofisa Uhusiano wa Takukuru, Mussa Misalaba amethibisha kuwa viongozi
hao walikamatwa kwa ajili ya uchunguzi
ambapo amesema kuwa Jamal Malinzi na wengine wanaendelea kuhojiwa
kwa tuhuma mbalimbali.
Kuhusu ufafanuzi wa tuhuma hizo, ofisa huyo alikataa kuzitaja kwamba ni suala la kiuchunguzi.
Kuhusu ufafanuzi wa tuhuma hizo, ofisa huyo alikataa kuzitaja kwamba ni suala la kiuchunguzi.
Pia alipoulizwa sasa ni lini viongozi
hao watafikishwa mahakamani alisema hawezi kusema kwani inawezekana kama
watuhumiwa hao wakitoa ushirikiano kwa Takukuru wa ushahidi wanaweza
wasifikishwe mahakamani.
0 COMMENTS:
Post a Comment