June 28, 2017Mshambuliaji wa  Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo katika Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Ngoma ambaye alikuwa akihusishwa kujiunga waponzani wa Yanga, Simba kabla ya kuzuka kwa taarifa za kujiunga na klabu ya Polokwane City inayoshiriki Ligi ya kuu ya Afrika Kusini 'Primiership ABS' ambapo alitua nchini usiku wa jana na  mchana  wa leo amesaini mkataba huo.

3 COMMENTS:

 1. Salehe nadhani Leo na gazeti lako mmeumbuka, acha maneno, ikubali yanga tu kiaina haina namna. Ulipanga mpaka kikosi chako cha kwenye gazeti LA champion akiwa ndani pia sasa Leo umeumbuka.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Acha kumwaga povu,vyombo vya habari vina mchango mkubwa sana katika kuipandisha thamani ya mchezaji,yawezekana Yanga walitaka kumsainisha kwa milioni 10 tu,lakini kutokana na taarifa za vyombo vya habari,tetesi za mchezaji husika kutakiwa pia na klabu nyingine hasimu,kunaifanya klabu yake kuongeza dau ili imbakishe.Kama si vyombo vya habari,Mkude wa Simba asingesajiliwa kwa mamilioni aliyopewa.

   Delete
  2. Wewe hujui kitu acha kumtetea huyo Saleh kwa usimba wenu,mmeumbuka sasa!

   Delete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV