June 23, 2017Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), litatoa ushirikiano wa kutosha wakati klabu ya Everton itakapotua nchini.

Uongozi wa TFF, umetoa neema ziara ya Everton ambayo inakuja nchini kuandika rekodi kuwa timu ya kwanza ya England kufanya maandalizi ya msimu mpya nchini Tanzania.
Everton watawasili nchini Julai 12 na siku inayofuata Julai 13 watashuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kucheza na Gor Mahia ambao ni mabingwa wa SportPesa Super Cup.

Mkurugenzi wa wa Ufundi TFF, Salum Madadi amesema wataungana na wenyeji wa Everton kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.

“Ujio wa Everton ni jambo kubwa sana kwa soka la Tanzania. Tunaamini kutakuwa na mafunzo na tutaungana nao kuwa sehemu ya washiriki wa karibu.

“Everton ni timu maarufu England na duniani kote. Hivyo kuna nafasi ya kujifunza wanapokuwa hapa nchini,” alisema Madadi.

Pamoja na hivyo, Madadi amewaomba mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya Julai 13 kushuhudia mechi hiyo lakini pia kuwaonyesha Everton, Tanzania ni nchi ya wapenda soka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV