June 5, 2017


Kiungo wa zamani wa Newcastle, Cheick Tiote ameanguka ghafla na kupoteza maisha akiwa mazoezini.

Tiote amepoteza maisha akiwa na umri wa miaka 30, alikuwa mazoezini katika kikosi cha Beijing Enterprises kinachoshiriki ligi daraja la pili.
Kiungo huyo raia wa Ivory Coast amejiunga na timu hiyo miezi mine tu iliyopita.

Alikimbizwa hospital zikiwa ni juhudi za kuokoa maisha yake lakini haikuwezekana.

Tiote amewahi kuwa kiungo tegemeo wa timu ya taifa ya Ivory Coast iliyokuwa inaongozwa na Didier Drogba.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV