Baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Njombe Mji, Azam FC sasa inakwenda mkoani Iringa kuendelea na ziara ya kujiandaa na msimu mpya.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema wamekubali kipigo hicho kutoka kwa Njombe na sasa wanaendelea na ziara hiyo.
“Lengo letu ni kujifunza kutokana na tunachojifunza kutokana tunachopata katika mechi za kirafiki.
“Tunaendelea na ziara yetu Nyanda za Juu Kusini. Sasa tunakwenda Iringa kucheza na Lipuli ambayo pia iko Ligi kuu Bara,” alisema.
Katika mechi ya leo mjini Makambako, Njombe ilionyesha soka safi ikiongozwa na Ditram Nchimbi aliyejiunga nayo akitokea Majimaji ya Songea.
Yaan salleh hata blog duh, sasa simba anahusikaje hapo kaka.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDelete