July 12, 2017


Pamona na kwamba msimu ujao Abdi Banda hatakuwepo katika kikosi cha Simba, lakini amefunguka kuwa kikosi hicho kitatisha zaidi kutokana na kusajiliwa kwa wachezaji mahiri kama Emmanuel Okwi na John Bocco.

 Banda ambaye amemaliza mkataba wake Simba, msimu ujao atavaa jezi za Baroka FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini ambapo amesema nyota hao wawili aliowataja, ndiyo watakaoisumbua Yanga wakikutana. 

Simba katika kipindi hiki cha usajili, imesajili nyota kadhaa akiwemo Bocco na Okwi ambao wanatajwa kuwa wataibeba timu hiyo msimu ujao pamoja na Aishi Manula.

Banda alisema anawapongeza viongozi wa Simba kutokana na kufanya usajili wa maana, hivyo anaiona timu hiyo ikitamba msimu ujao. 

“Simba imefanya usajili wa maana na wa uhakika, kitendo cha kumchukua Bocco na Okwi naamini msimu ujao timu itakuwa imara zaidi na kufanya makubwa. 


“Naweza kusema kwamba msimu ujao hakuna wa kuizuia Simba, hao Yanga wasubiri maumivu kutoka kwa Bocco na Okwi,” alisema Banda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV