July 12, 2017
KAJUNA (KUSHOTO), SIKU ALIPOMPOKEA KIONGERA.

Kaimu Makamu Rais wa klabu ya Simba, Iddi Kajuna yuko nchini Ghana kumalizana na mshambuliaji Thomas Gyan.

Gyan anaelezwa kuwa ni mdogo wa Asamoh Gyan ambaye ni mwanasoka nyota wa Ghana.

Chanzo kimeeleza Kajuna jana alishuhudia mechi Gyan akicheza na baada ya hapo ataangalia kama wamalizane au vipi.

“Ilikuwa ni kama kuhakikisha tu lakini naona kama atamalizana naye hata kabla ya kuja jana,” alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV