July 12, 2017
Ligi Kuu Bara msimu ujao itawakutanisha vigogo Simba na Yanga Oktoba 14 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Lakini kabla watani hao watakutana Agosti 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ngao ya Jamii ambao huchezwa wiki moja kabla ya kufunguliwa kwa Ligi Kuu Bara.

Ligi Kuu Bara msimu wa 2017-18 inatarajia kuanza rasmi Agosti 26, 2017 na kufikia tamati Mei 20, 2018.

Watani hao wa jadi watakapokutana Oktoba, Simba ndiyo watakuwa wenyeji wakati Yanga watakuwa wenyeji katika mechi ya mzunguko wa pili itakayochezwa mwakani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV