July 22, 2017



Sahau kuhusiana na Kipa Ally Mustapha ‘Barthez’ aliyesajiliwa na Singida United, timu hiyo imemweka mkononi kiungo mshambuliaji Deus Kaseke aliyemaliza mkataba na Yanga.

Kocha wa Singida United, Hans van Der Pluijm raia wa Uholanzi, ameweka wazi kuwa ana furaha kubwa msimu ujao kufanya kazi na Kaseke aliyewahi kufanya kazi wakiwa Yanga msimu uliopita. 

Jana Ijumaa Kaseke aliliambia Championi Jumamosi kuwa; “Muda wowote nasaini Singida United, halafu kesho (leo) naenda Mwanza kambini kuungana na wenzangu, hii imekuja baada ya kushindwana na Yanga katika kuongeza mkataba.”

Kaseke anasaini miaka miwili kucheza Singida United ambako ataungana na Barthez, ambaye walicheza wote msimu ulioita Yanga na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.


Pluijm ameliambia gazeti hili kwamba: "Kaseke yupo njiani anakuja Singida United, naweza kusema huyu ni kati ya vijana ambao wanajielewa na wanajua majukumu yao wawapo uwanjani, nafurahi kufanya naye kazi tangu nikiwa Yanga na sasa anakuja huku.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic