July 30, 2017
Mshambulizi mpya wa Difaa Al Jadid, Simon Msuva ameanza vizuri kwa kufunga bao safi. Timu hiyo inashiriki Ligi Kuu ya Morocco.

Msuva ameanza kwa kufunga bao katika mechi ya kirafiki waliyocheza leo ingawa Difaa Al Jadid walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.

“Kweli nimefunga bao moja ingawa tumepoteza, namshukuru Mungu nimeanza vizuri,” alisema Msuva ambaye amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu.


Msuva alitua nchini humo siku nne zilizopita kabla ya kusaini mkataba na kuanza mazoezi moja kwa moja..

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV