July 9, 2017


Mtangazaji za kituo cha redio cha EFM, Seith Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma, amefariki dunia leo katika Hospitali ya Taifa MuhimbiliKwa mujibu wa baadhi ya wafanyakazi wenzake ambao hawakutaka kutajwa majina yao kwa vile siyo wasemaji, walisema marehemu alianza kuugua kiasi cha mwezi mmoja uliopita na msiba uko nyumbani kwa baba yake mzazi huko Changanyikeni.Marehemu ambaye alikuwa akitangaza kipindi cha Ubaoni, kinachorushwa na redio hiyo kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, saa kumi jioni, alikuwa pia ni bloga maarufu katika mitandao ya kijamii.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV