July 29, 2017


Pamoja na Arsenal kuitwanga Benfica kwa mabao 5-2 katika mechi ya kirafiki, bado kuna mashabiki hawamtaki katika klabu hiyo.

Shabiki mmoja alifanikiwa kupenya uwanjani wakati wa mchezo huo na kusema maneno makali dhidi yake akionyesha kumpinga kwake.

Hata hivyo shabiki huyo aliondolewa uwanjani na askari baada ya kuwa ameropoka maneno hayo makali dhidi ya Wenger.

Miezi michache iliyopita, Wenger aliongeza mkataba wa miaka miwili kuifundisha Arsenal licha ya kuwa mashabiki wakionyesha wazi hawamtaki au wamemchoka.

Raia huyo wa Ufaransa alianza kuifundisha Arsenal tokea mwaka 1996 akitokea Grampus Eight ya  Japan.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV