July 27, 2017


Jumatano ya July 26 2017 zilienea taarifa za kukamatwa na TAKUKURU kwa mwenyekiti wa chama cha mpira Dar es Salaam DRFA Almas Kasongo, mgombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya TFF kanda ya Dar es Salaam na mchambuzi wa habari za michezo Tanzania Shaffih Dauda pamoja na wanafamilia wengine wa mpira Mwanza.




Taarifa zilizokuwa zimeripotiwa kukamatwa kwa watu hao zinadai ni viashiria vya rushwa na kuhusishwa na kampeni za chini kwa chini za uchaguzi Mkuu wa TFF, hivyo TAKUKURU ikawakamata kwa mahojiano yaliyodumu kwa saa kadhaa kabala ya kuwaachia kwa dhamana.

Baada ya kurejea Dar es Salaam akitokea Mwanza Shaffih Dauda alipokuwa amekwenda na viongozi wa DRFA kwa ajili ya uzinduzi wa Ndondo Cup kupitia Clouds FM ameeleza tukio la kukamatwa kwao lilivyokuwa ambalo linadaiwa kulenga kuwachafua katika uchaguzi Mkuu wa TFF.


“Nimehojiwa na TAKUKURU nikiwa Mwanza kwa ajili ya uzinduzi wa Ndondo Cup ambayo inaweza kuanza Mwezi wa 9, nilichogundua ni siasa za uchaguzi wa TFF, nilikutana na viongozi wa mpira Mwanza kwa ajili ya mipango ya Ndondo Cup Nilikua na viongozi wa DRFA tulioanzisha nao Ndondo Dar,” Shaffih Dauda.


“Viongozi wa DRFA walikuwepo Mwanza kuwaeleza uzoefu viongozi Mwanza kabla hawajafanya na wao mwaka huu, baadhi ya watu na mawazo yao walitoa taarifa za uongo na kufanya mipango ya hovyo wakijua nafanya mipango ya uchaguzi, sigombei TFF kutaka cheo, nagombea kuleta mabadiliko kwenye soka, ndio maana napambana kupeleka Ndondo Cup kila sehemu,” Shaffih Dauda.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic