July 26, 2017
Wakati kuna picha ainasambaa mitandaoni kwamba tayari mshambuliaji wa pembeni, Simon Happygod Msuva, rasmi amejiunga na Difaa Al Jadid ya Morocco, mwenye amesema si kweli.

Kumekuwa kuna picha inayozagaa mitandaoni ikionyesha tayari Msuva amejiunga na timu hiyo ya Morocco Kaskazini mwa bara la Afrika.

Lakini Msuva ameiambia SALEHJEMBE kuwa ndiyo yuko airport akijiandaa kuondoka kwenda Morocco na si kweli kama inavyoelezwa.

Taarifa nyingine zinaeleza, baada ya kutua Morocco, tayari Al Jadid imemuandalia Msuva mkataba wa miaka mitatu ambao utamalizika mwishoni mwa msimu wa 2019-20.

Jana, Msuva alifika katika mazoezi ya Yanga na kuwaaga wachezaji na makocha wa Yanga kabla ya kuanza safari yake hiyo kwenda Morocco kuanza maisha mapya.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV