July 18, 2017


Mashabiki wa soka wa Tanzania wamepata bahati ya pekee kutazama ‘live’ mechi za kujiandaa na msimu ujao wa michuano ya Kombe la Ubingwa Kimataifa (ICC) kupitia King’amuzi cha StarTimes.

Michuano hiyo itakayozihusisha timu kutoka ligi tano kubwa za Ulaya zikiwemo Real Madrid, Barcelona, Bayern Munich, Manchester City na Manchester United zitachezwa katika nchi tatu ambazo America, Singapore na China.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa StarTimes Tanzania, Juma Suluhu, michuano hiyo ya ICC itaonyeshwa kupitia chaneli tano za michezo zilizomo katika King’amuzi cha StarTimes kuanzia jana Jumanne.

Juma alisema wanajivunia kuonyesha ‘live’ michuano hiyo inayojumuhisha timu kutoka ligi tano bora za Ulaya zitakazopambana kumpata aliye bora zaidi.

“Tumewaletea tena wateja wetu nafasi ya pekee ya kutazama mechi za michuano ya ICC kupitia StarTimes, ni burudani nyingine ya kipekee wakati huu ambapo ligi zimesimama,” alisema Juma.

“Ni wakati wa kuzitazama timu bora zenye wachezaji bora. Kutakuwa na mechi 18 zitakazojumuhisha klabu 14 katika viwanja 15 katika nchi tatu, hili ni tukio la aina yake.

“Ligi zikisimama si kila kitu cha soka kisimame, kupitia michuano hii tukayoonyesha moja kwa moja, mashabiki watapata fursa ya kutazama mechi ya El Clasico na nyingine za Manchester United, Chelsea na Bayern Munich,” alisema Juma.


StarTimes ni king’amuzi pekee kilichopata haki za kurusha ‘live’ michuano hiyo ya ICC kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara. StarTimes pia itarusha ‘live’ michuano yote ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) msimu wa 2017/18  ikiwemo Kombe la Dunia Urusi 2018.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic