July 18, 2017


Baada ya kuwa kimya kwa muda mwingi, Njombe Mji wameanza usajili kwa kumnasa mshambuliaji Ditram Nchimbi kutoka Mbeya City.

Njombe Mji ambao wamepanda daraja hadi Ligi Kuu Bara, wamekuwa kimya kwa muda mrefu kuhusiana na usajili.


Mwenyekiti wa Njombe Mji, Erasto Mpete amethibitisha wao kumnasa Nchimbi kwa mkataba wa miaka miwili.

Nchimbi alijiunga na Mbeya City mwaka 2015 akitokea Majimaji ya Songea.

Pamoja na kwamba hajafunga mabao mengi ni kati ya washambulizi wasumbufu anapokuwa uwanjani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic