July 31, 2017



Mashabiki wengi wa soka nchini, wametuma maoni yao wakiipongeza StarTimes kupitia king'amuzi chake kuonyesha michuano ya ICC mwanzo hadi mwisho.


Mashabiki hao kupitia mitandao mbalimbali ya Salehjembe, wamefurahishwa na namna ambavyo wameweza kuwaona wachezaji wapya wa timu mbalimbali kama Arsenal, Real Madrid, Barcelona, Man United, Man City na timu nyingine wakati wa maandalizi ya msimu mpya.

Wachezaji hao wameonekana katika michuano ya ICC na StarTimes ilirusha kupitia mfumo wa HD ambao unamfanya mtazamaji apate hisia za kuwa uwanjani.


Mashabiki hao pia walifurahia bei nafuu ya ving'amuzi huku wakifaidi michuano hiyo mitamu.

Moja ya mechi zilizofunga dimba la ICC ni ile iliyochezwa Miami nchini Marekani na kuwakutanisha vigogo wa El Clasico, Real Madrid dhidi ya Barcelona.

Katika mchezo huo uliopigwa mjini Miami Marekani, kwenye Uwanja wa Hard Rock, ni kati ya ile ya kujiandaa na msimu lakini huu ulikuwa unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani kote. Barcelona walishinda kwa mabao 3-2.

Hizi ni timu mbili zenye upinzani mkubwa zaidi kwenye Ligi Kuu ya Hispania, La Liga.

Lionel Messi, ambaye ni kati ya wachezaji bora zaidi duniani kwa sasa alionyesha kiwango cha hali ya juu sana.

Huu unatajwa kuwa mchezo wa kwanza mkali zaidi wa El Clasico kupigwa nje ya nchi ya Hispania.

Gerard Pique, naye alionyesha kiwango kizuri kwenye mchezo huo ambao ulipigwa mbele ya watazamaji 66,000 na kurushwa mubashara na Startimes.


Timu zote mbili zilijaza vikosi imara kwenye mchezo huo.

Staa wa Barcelona, Neymar alitoa pasi mbili za mabao kwenye mchezo huo huku akifanikiwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu.

Barcelona walifanikiwa kujipatia mabao yao kupitia kwa Messi, Ivan Rakitic na  Pique.

Huku Madrid wakifunga kupitia kwa Mateo Kovacic na Marco Asensio.

“Ni mchezo sawa na michezo mingine ya maandalizi naamini kuwa mashabiki wetu wameshuhudia nini ambacho kimetokea uwanjani na naamini kuwa timu yetu imeonyesha kiwango kizuri.


“Tulikuwa tunataka matokeo, lakini yanayoonyesha kuwa kuna kitu tunakifanya kabla msimu wa ligi haujaanza, naamini kuna picha imeonekana,” alisema kocha wa Madrid, Zinedine Zidane.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic