August 12, 2017

MMILIKI wa klabu ya Newcastle, Mike Ashley amemweleza kocha wa timu hiyo, Rafa Benitez kuwa klabu hiyo haina fedha za usajili.


Benitez ambaye alishuka na timu hiyo alipambana na kuhakikisha kuwa inapanda tena kwenye Ligi Kuu England, lakini amekuwa akilalamika kuwa mmiliki wa timu hiyo alimdanganya kuwa atampa fedha za kutosha za usajili.“Hatuna fedha na Benitez anajua, tumetumia kitita cha pauni milioni 31 zinatosha kabisa, hatuwezi kupambana na timu kubwa kwenye usajili,” alisema Ashley.

  

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV