August 12, 2017
WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr, Harrison Mwakyembe amesema anaamini presha zimekuwa za kupanda na kushuka kwa wagombea na wajumbe wa Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania lengo likiwa ni kuhakikisha kupata viongozi bora.

Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unafanyika leo mjini hapa kwenye Ukumbi wa St Gasper kwa ajili ya kuwapata washindi wa nafasi ya urais, makamu wa rais na wajumbe wa kamati ya utendaji.

Uchaguzi huo unasimamiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Revocatus Kuuli unafanyika baada ya Jamal Malinzi kuelekea kumaliza kipindi chake cha uongozi cha miaka minne.

Mwakyembe anasema: “Ninajua presha imekuwa ya kupanda na kushuka siyo tu kwa wagombea bali na wajumbe na ninajua ni kwa nia nzuri tu ya kupata viongozi bora na adhimu kwa maendeleo ya soka nchini Tanzania.

“Viongozi bora huibuliwa na wajumbe makini wanaoongozwa na dhamira njema na uzalendo usiotetereka kwa vishawishi vya mpito.


“Serikali inaamini tuna wajumbe makini, wasioyumbishwa kwa vishawishi vya muda, mpito wanaoongozwa na dhamira njema na uzalendo wa hali ya juu ambao watatuibulia viongozi bora wa TFF wenye ari na moyo.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV