August 3, 2017Baada ya Yanga kuitwanga Moro Kids kwa mabao 5-0 katika mechi yao ya kirafiki, Kocha George Lwandamina ameonyesha kufurahia mwanzo huo.

Lwandamina amefurahishwa kutokana na kuona mambo mengi aliyowafundisha mazoezini katika kuwekeza mifumo yake mipya.

“Kocha ameonekana kufurahia sana. Ishu si kwamba mabao matano, lakini kocha anachoangalia ni namna mifumo yake ilivyofanya kazi.

“Unajua sasa kikosi kina wachezaji kadhaa wapya ambao wanapaswa kuchanganywa pamoja ili kutengeneza timu moja imara.

“Walivyocheza kwa asilimia kubwa ni kile anachokitaka kocha na amekiona kinafanyika,” kilieleza chanzo kutoka ndani ya kambi ya Yanga.


Yanga ambayo ipo kambini mjini Morogoro ilicheza kwa vikosi viwili tofauti ikianza na cha kwanza katika dakika 45 za kwanza kabla ya kubadili kikosi chote katika dakika 45 za mwisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV