August 3, 2017


Raphael Daud ameonyesha kuwa atakuwa msaada mkubwa katika kikosi cha Yanga.

Hii ni baada ya kucheza dakika 45 zake za kwanza katika mechi ya kirafiki dhidi ya Moro Kids ya Morogoro na kufanikiwa kufunga bao.

Pamoja na kufunga bao, Raphael alionyesha uwezo mkubwa hasa katika kuchezesha timu.

Kiungo huyo kinda aliyejiunga na Yanga akitokea Mbeya City, alikuwa akitumia muda mwingi kugawa mipira huku akiomba na kurejesha kwa wenzake.

Pia alikuwa akipiga pasi fupi na ndefu za haraka na kuonyesha kuwavutia wengi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV