August 2, 2017Benchi la ufundi la kikosi cha Difaa Al Jadid limeonyesha kutoridhishwa na mchezaji Ramadhani Singano.

Mmoja wa mawakala wanaotambulika na Fifa walioshughulikia safari ya Singano kwenda Morocco wamesema, mmoja wa makocha amewaambia benchi zima la ufundi limeona Singano hana tofauti na wachezaji wawili walionao.

“Wachezaji wawili walionao wanaonekana kama wanafanana sana na Singano. Hivyo wanaona kama hakuna jipya sana,” chanzo hicho kimeeleza.

Wakati chanzo hicho kimeeleza hayo, kuna taarifa Singano anaweza kurejea nchini kwa kuwa mkataba wake ulikuwa ni wa makubaliano ya awali.

Singano aliichezea Difaa Al Jadid kwa dakika 45 ikafungwa mabao 2-0. Kipindi cha pili kocha akabadili kikosi kizima na Mtanzania mwingine, Saimon Msuva akacheza na kufunga bao moja na mwisho matokeo yakawa 2-1.

SALEHJEMBE


1 COMMENTS:

  1. Kama mambo si mazuri kwake ni bora akarudi mapema awahi dirisha la usajili wa ndani ili apate timu ya kucheza,tatizo la huyo dogo anapotezwa na washauri wake,anapenda sana kurumbana na waajili wake anapotaka kuhama timu.Anasahau kuwa nyumbani ni nyumbani na unaweza kurudi muda wowote pale unaposhindwa kufanikiwa kule ulipoenda kujaribi bahati yako.Aligombana na Simba,akawatusi Azam sasa nadhani aje ajaribu bahati yake Lipuli au Mji Njombe,vinginevyo benchi litamuhusu

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV