August 12, 2017



Mshambulizi nyota wa Yanga, Obrey Chirwa naye ni majeruhi kutokana na maumivu ya mguu.

Chirwa raia wa Zambia, hatacheza mechi za kirafiki na mazoezi analazimika kuendelea kupata matibabu.

Imeelezwa Chirwa anaungana na kundi la kipa Beno Kakolanya na kiungo wa pembeni wa Yanga, Geofrey Mwashiuya ambao pia ni majeruhi.

Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh amethibitisha lakini amesema wanaendelea vizuri.

"Mnapoanza mazoezi, au wakati mnaendelea, suala la majeruhi ni kawaida kabisa. Lakini wote wanaendelea vizuri," alisema Hafidhi.

"Matumaini yetu hivi karibuni watakuwa fiti kabisa kwa kuwa kitengo cha tiba kinaendelea kufanya kazi yake."

Yanga imekuwa ikiendelea kufanya mazoezi ya nguvu chini ya Kocha George Lwandamina ili iweze kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Bara pamoja na kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic