August 20, 2017


Nahodha wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard amemcharukia kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil kwamba hana juhudi za kutosha kuisaidia timu yake.
Ozil alikuwa katika kikosi cha Arsenal wakati timu hiyo ilipolala kwa bao 1-0 dhidi ya Stoke City na kupoteza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu England ikiwa ndiyo mechi ya pili kwa msimu huh mpya.
Gerrard ambaye ni mchambuzi katika runinga ya BT Sport amesema wachezaji wakubwa wa Arsenal hasa Ozil hawakuonyesha juhudi za kutosha.
Badala yake, Gerrard amemtaka Ozil kuonyesha juhudi zaidi kwa kuwa ana uwezo mkubwa ambao kama atautumia kwa juhudi atakuwa msaada maradufu kuliko sasa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic