Wanachama na mashabiki wa Simba wilayani Muheza, Tanga wameonyesha uungwana kwenda kuchangia damu kwa ajili ya watoto katika hospitali ya wilaya hiyo.
Awali ilielezwa kulikuwa na upungufu wa damu kwa wagonjwa katika hospitali hiyo na wanachama na mashabiki hao wakaungana kwenda kushiriki zoezi hilo.
Ukiachana na wanachama hao kuchangia damu, pia walitoa vinywaji na vitafunwa kwa watoto wagonjwa waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo.
MHARIRI:
Salehjembe inawapongeza wanachama na mashabiki hao kwa moyo wa kizalendo ambao unaonyesha kiasi gani mpira unaweza kusaidia watu bila ya kufuata itikadi ya ushabiki na kadhalika.
Wengine pia katika sehemu nyingine nchini wanaweza kufanya hivyo.












0 COMMENTS:
Post a Comment