HAKUNA namna kwani Yanga imebidi ikubali kucheza mechi ya kirafiki
dhidi ya Ruvu Shooting, leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Azam Complex
uliopo Chamazi, Mbagala nje kidogo ya Dar es Salaam.
Awali Yanga na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) walikuwa wagumu kupeleka mechi za timu hiyo kwenye uwanja huo kutokana na sababu za kiusalama lakini jana walikubali baada ya kukosa uwanja. Mwanzo mipango ilikuwa mechi hiyo ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara ichezwe kwenye Uwanja wa Taifa, lakini ikashindikana kutokana na uwepo wa shughuli za kiserikali uwanjani hapo siku hiyo.
Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, aliliambia Championi Jumamosi jana kuwa, wamewaomba Azam FC kuutumia uwanja wao kwa mechi hiyo baada ya kukosa uwanja.
“Tumepokea taarifa asubuhi ya leo (jana) kutoka kwa serikali juu ya kusitishwa kuutumia Uwanja wa Taifa Jumamosi kwa mechi yetu, kutokana hali hiyo tumewaomba Azam na wamekubali.
“Mechi hii itaanza saa 10:00 jioni na kiingilio kitakuwa shilingi 7,000 na 5,000, hivyo tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza na tunaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi. “Pia nichukue nafasi hii kuwashukuru Azam kwa kumruhusu mchezaji wao, Gadiel Michael kuja kuchezea Yanga kwani ni jambo la kiungwana,” alisema Mkwasa.
Baada ya mechi hiyo, Yanga, kesho Jumapili itakwenda Zanzibar ambapo usiku itacheza mechi ya kirafiki na Mwandege FC kwenye Uwanja wa Amaan na Jumatatu asubuhi itaenda kambini Pemba kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba Agosti 23, mwaka huu.
CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:
Post a Comment