TOFAUTI na miaka
iliyopita ya rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuapishwa siku chache
baada ya uchaguzi lakini leo hapa Dodoma ambapo unafanyika uchaguzi, rais
ataapishwa muda mfupi baada ya kushinda.
Uchaguzi
Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unafanyika leo mjini hapa kwenye
Ukumbi wa St Gasper kwa ajili ya kuwapata washindi wa nafasi ya urais, makamu
wa rais na wajumbe wa kamati ya utendaji.
Uchaguzi huo
unasimamiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Revocatus Kuuli
unafanyika baada ya Jamal Malinzi kuelekea kumaliza kipindi chake cha uongozi
cha miaka minne.
Waziri wa
Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr, Harrison Mwakyembe amesema hayo leo
alipokuwa akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu na waandishi wa habari.
Mwakyembe amesema
rais na wajumbe watakaopatikana leo wataapishwa mbele ya wapiga kura wote wa
uchaguzi tofauti na miaka ya nyuma ambapo walikuwa wakishahau haki ya
waliowachagua kwa kuwaapisha nje ya utaratibu.
0 COMMENTS:
Post a Comment