Juuko Murshid amerejea nchini na kujiunga na timu yake ya Simba.
Kurejea kwake kumekuwa na taarifa nyingi likiwemo suala la kwamba amefanya majaribio na kufeli, lakini ukweli ni kwamba, Simba na Orlando Pirates ya Afrika Kusini hawakuelewana vizuri.
Klabu ya Orlando ilitaka Juuko akafanye majaribio na Simba wakaona kama kulikuwa na ujanja fulani. Kwa kuwa Juuko ni beki aliyecheza michuano ya Kombe la Mataifa Afrika.
“Baada ya kuwa kuna huo mzunguko, Juuko alibaki tu Uganda. Ilipoonekana hakuna wanachofanya Orlando ndiyo unamuona amerejea hapo,” kilieleza chanzo.
0 COMMENTS:
Post a Comment