August 15, 2017




Klabu ya Ndanda FC ya mkoani Mtwara leo imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya Motisun Group kupitia kwa bidhaa yao ya Kiboko.

Hiyo ikiwa ni siku chache lanka ya Ligi Kuu Bara ianze kutimua vumbi Agosti 26, mwaka.

Akizungumza na jijini Dar, Mshauri wa Masoko na Biashara wa Ndanda, Peter Simon alisema wanaushukuru udhamini huo ambao utawasaidia wao kupambana na mikikimikiki ya ligi kuu kwenye msimu ujao ambao anaamini utakuwepo mkubwa. 



Simon alisema, udhamini utawawezesha wao timu yao kusafiri nje ya mikoa kwa ajili mechi za ugenini huku wakiahidi kutowaangusha kwa kipindi hicho cha mwaka mmoja. 

"Niwaahidi Motisun Group kupitia kwa bidhaa yao ya Kiboko kuwatangaza vema kupitia timu yao itakayoshiriki ligi kuu. 

"Ndanda tunaamini kuwa kupitia timu yetu wataongeza idadi ya wateja kutokana kuwatangaza vema, "alisema Simon. 

Kwa upande wa Motisun kupitia kwa Mkuu wa Masoko, Edward Mlyansi alisema kuwa "Kwa kuanza wanaanza na udhamini huo wa mwaka mmoja na baadaye watauboresha zaidi hapo baadaye.


"Kikubwa wanataka kuona timu ikipata matokeo mazuri na kuleta ushindani mkubwa na hatutaki kuona migogoro katika timu, "alisema Mlyansi.

1 COMMENTS:

  1. Mimi nawapongeza sana Ndanda kwa kupata udhamini huu. Vilabu vingine vichangamke maana hawa wadhamini hawaji wenyewe, wanatafutwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic