Wachezaji watatu Donald Ngoma, Ibrahim Ajibu na Amissi Tambwe wataanza katika mechi dhidi ya Simba.
Katika mazoezi ya Yanga mjini hapa, Kocha George Lwandamina amekuwa akiwapanga mara kadhaa kuhakikisha watengeneza umoja unaozalisha.
Hali hiyo inaonyesha washambulizi hao watatu wa aina tofauti, wataanza katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, wikiendi hii.
Yanga ipo kambini mjini Pemba kujiandaa na mechi hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.
0 COMMENTS:
Post a Comment