August 5, 2017Yule beki kisiki wa zamani wa Arsenal, Sol Campbell anatarajiwa kutua nchini leo Jumamosi mchana kwa mwaliko wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya SportPesa.

Campbell ambaye pia amewahi kuichezea Tottenham Hotspur ya England, akiwa nchini kesho atajumuika na baadhi ya wadau wa soka kutazama mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Arsenal na Chelsea.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Abbas Tarimba, akiwa nchini Campbell pia atafanya mafunzo kwa timu ya Magnet kwenye Uwanja wa Gymkhana na kutembelea timu ya Muungano kwenye Uwanja Karume ambako ataanzia ziara yake.

“Huyu ni nyota wa pili wa zamani wa soka baada ya Leon Osman wa Everton, tunajua bado watu wanakumbuka ujio wa Everton huu ni muendelezo wa kampuni yetu kuleta hamasa ya soka nchini,” alisema Tarimba.


Tarimba alisema SportPesa inaendelea kuwapa hamasa ya soka Watanzania kwa ujio wa nyota huyo ukiachana na udhamini iliyoutoa kwa Simba, Yanga na Singida United. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV