August 19, 2017




Kocha Mkuu wa Mlandege FC ya Zanzibar, Jaala Abdallah Salum amesema Yanga ipo vizuri kuliko Simba katika fiziki.

Salum ana nafasi ya kuzing'amua timu zote mbili kutoka Tanzania  Bara kwa kuwa zilicheza mechi za kirafiki dhidi yake.

Katika mechi ya kwanza, alikutana na Yanga ambao ni mabingwa wa Tanzania Bara na kulala kwa mabao 2-1 katika mechi ya pili, wakaikomalia Simba kwa sare ya bila kufungana.


Kwa matokeo hayo, Salum anaamini Yanga wako vizuri zaidi huku akiwaasa Simba kufanya mabadiliko kadhaa kabla ya kuivaa Yanga, Jumatano.

Yanga itawavaa Simba ambao ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho katika mechi ya Ngao ya Jamii itakayochezwa Jumatano ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Salum amesema timu yake ilitoka sare na Simba kutokana na fiziki yao kuwa juu kuliko wapinzani wao hali ambayo ni tofauti na walipocheza na Yanga.

“Mechi yetu na Simba ilikuwa nzuri kwetu kwani tuliwazidi katika fizikia maana wao ilioneka ipo chini tofauti na sisi, lakini Yanga walitusumbua kwa sababu walikuwa na fiziki kuliko sisi.

 “Yanga walikuwa fiti kuliko sisi walikuwa na nguvu na kasi katika muda wote wa mchezo, Kocha wa Yanga George Lwanda-mina ni mjanja sana kwa sababu alianza kuwatumia vijana, wakatu-chosha.


“Halafu akawaingiza wale ambao ni wazoefu ikawa shida kwetu ila kikubwa ilikuwa fizikia yetu ipo chini, nadhani Simba huenda katika siku hizi mbili wakawa vizuri kabla ya mchezo na Yanga vinginevyo itakuwa tabu kwao,” alisema Salum.

1 COMMENTS:

  1. Simba wasubiri supu ya mawe.....
    Hongera saleh jembe kwa HABARI ZAKO nzuri

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic