August 11, 2017




Mgombea nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Imani Madega na mgombea Ujumbe wa shirikisho hilo, Lameck Nyambaya wameahidi makubwa kama wakifanikiwa kushinda nafasi hizo.

Uchaguzi huo wa TFF unatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi mkoani Dodoma kwa wagombea nafasi mbalimbali za shirikisho hilo.

Akizungumza jijini Dar, Madega alisema kuwa taaluma yake ya sheria ni ‘silaha’ tosha ya kuliwezesha shirikisho hilo kuwa na nguvu na kuepuka kuingia mikataba isiyokuwa na tija.

Madega alisema kuongoza TFF inahitaji mtu mwenye muda kwa mujibu wa taratibu za Fifa na Caf na kuwaomba wagombea kuachana na wagombea wenye ajira kwani watakosa muda wa kulitumikia shirikisho hilo.

“Mimi ni mwanasheria wa kujitegemea, sipangiwi kazi, ni rahisi kulitumikia shirikisho kuliko wagombea wengine, rais wa TFF ndiye mtendaji mkuu, hivyo anatakiwa kupatikana muda wote, anatakiwa kuwa mkazi wa eneo ambalo ofisi kuu inapatikana,” alisema Madega.

Kwa upande wa Nyambaya yeye alisema: "Lengo langu ni kujenga TFF yenye uwezo mkubwa wa kifedha na kusaidia vyama vya mikoa ili kuleta maendeleo ya soka, kwa sasa kuna nafasi kubwa kutokana na serikali kuleta sera ya maendeleo ya viwanda ambavyo vitawekeza hapa nchini.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic